Yahya
Jammeh aliyeitawala Gambia kwa miaka 22, hatimaye jana aliondoka nchini
humo na kwenda kuishi uhamishoni baada ya kushindwa katika uchaguzi
mkuu wa Disemba Mosi mwaka jana.Jammeh alishindwa na kiongozi aliyekuwa
akiungwa mkono na vyama vya upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa
akiishi nchni Senegal alipoapishwa kuwa Rais wa Gambia baada ya Jammeh
kukataa kutoka madarakani awali. Yahya Jammeh alipokuwa akiiongoza Gambia
aliweza kujinunulia vitu vingi vya kifahari na moja wapo ni gari lake
la kifahari aina ya Rolls Royce.
Gari hili
ambalo kwenye viti vyake ameandika jina lake, lina thamani ya kati ya
fedha za kitanzania milioni 500 hadi milioni 800. Rolls Royce ni moja ya
magari ya kifahari na ya kipekee duniani ambayo mara nyingi hutumiwa na
watu wenye uwezo mkubwa kifedha.
Gari hili
la Yahya Jammeh liliwashangaza rais wengi wa Gambia lilipokuwa
likikatisha katika viunga vya mji wa Banjul kumpeleka kiongozi huyo
uwanja wa ndege tayari kuondoka nchini humo.
Licha ya
kuwa Jammeh aliondoka nchini Gambia jana huku wananchi wakishangilia kwa
furaha, imeelezwa kuwa kiongozi huyo alikomba fedha katika hazina ya
nchini hiyo na kuiacha katika ukata mkubwa wa fedha.Taarifa kutoka
katika kambi ya Rais Adama Barrow zinaeleza kuwa dola za kimarekani
milioni 11 zilichukuliwa katika hazina ya nchi hiyo.Yahya Jammeh tayari
amewasili nchini Equatorial Guinea ambapo ndipo ataishi.
Hapa chini ni picha zaidi za gari hilo la kifahari;
Hapa ni
sehemu ya magari ya Yahya Jammeh yalipo uwanja wa ndege wa Banjul
Gambia, baada ya ndege toka Guinea kuzuiliwa kuyachukua.
No comments:
Post a Comment