Rais Yahya Jammeh wa Gambia
Muungano
wa Afrika AU umesema kuwa utawacha kumtambua Yahya Jammeh kama rais wa
Gabon kuanzia tarehe 19 Januari wakati muda wake utakapokamilika.
Baraza la
amani na usalama la muungano huo pia limetishia kuchukua hatua kali
iwapo vitendo vya Jammeh vitasababisha mauaji ya raia wasio na hatia.
Muungano huo pia umevitaka vikosi vyake vya kulinda amani kujizuia.
Rais wa
Nigeria Muhammadu Buhari yuko nchini Gambia akiongoza ujumbe wa mataifa
ya magharibi ECOWAS katika jaribio la hivi karibuni kumshawishi bwana
Jammeh kuwachilia mamlaka kwa Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa
urais mwezi uliopita.
Adama Barrow na Yahya Jammeh
Bwana
Barrow ameambia BBC kwamba ataapishwa kama rais wiki ijayo na kumtaka
Jammeh ashiriki katika mazungumzo na wapatanishi hao.
Aidha
memtaka Rais anayemaliza muda wake Yahya Jammeh kushiriki katika
mazungumzo ya moja kwa moja ili kutatua mgogoro wa kisiasa ulioikumba
nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment