Alieu Momar Njai,
Mwenyekiti
wa Tume ya uchaguzi nchini Gambia, Alieu Momar Njai, ameondoka nchini,
kwa mujibu wa ripoti kadhaa. Familia yake imefahamisha BBC kuwa hayupo
nchini Gambia, na kamwe haitofichua eneo ambapo amekimbilia .
Inaarifiwa
kuwa Alieu Momar Njai alikimbilia mafichoni kufuatia vitisho vya kuuawa
baada ya kutangazwa kushindwa kwa Yahya Jammeh katika uchaguzi wa
urais.
Rais
anayemaliza muda wake kwa mara ya kwanza alikubali kushindwa na
kupongeza ushindi wa mpinzani wake Adama Barrow, lakini baadae alipinga
ushindi huo na kuitaka mahakam kufuta matokeo ya uchaguzi wa urais,
akisema uchaguzi uligubikwa na kasoro nyingi.
Tume ya Uchaguzi ilitangaza kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Kufunguliwa upya kwa ofisi za Tume ya Uchaguzi
Makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yalifunguliwa wiki iliyopita kwa uamuzi wa serikali ya Gambia.
Desemba
13, makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yalifungwa na kuzingirwa na vikosi
vya usalama, kutokana na hatari ya kuchomwa moto, serikali imetangaza.
Serikali imeongeza kuwa "vikosi vya usalama vitasalia katika hilo.
No comments:
Post a Comment