Mazungumzo ya Geneva sita juu ya mgogoro wa
Syria, ambayo yalifanyika chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa,
yamemalizika bila kufikiwa natija iliyotarajiwa kwa ajili ya kukomesha
mgogoro wa nchi hiyo.
Mazungumzo
ya Geneva sita yalianza kuanzia tarehe 16 ya mwezi huu na kuhitimisha
shughuli zake siku nne baadaye. Mazungumzo hayo yalijikita katika nukta
nne muhimu, kupambana na ugaidi, kujitawala, katiba na uchaguzi. Pamoja
na hayo mazungumzo ya Geneva sita kama yalivyokuwa mazungumzo mengine ya
Astana, hayakuwa na faida kwa ajili ya kutatua mgogoro wa taifa la
Syria. Tatizo la kwanza lililoibuka katika mazungumzo ya Geneva sita ni
kwamba hayakujikita katika maudhui moja maalimu.
Kwa mfano tu Staffan de Mistura, mjumbe
wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria yeye alitaka kufanyike
mazungumzo kuhusiana na katiba ya mustakbali wa nchi hiyo, huku serikali
ya Damascus nayo ikikubaliana na pendekezo hilo la mjumbe wa Umoja wa
Mataifa. Hata hivyo makundi ya upinzani yalitaka kabla ya lolote lile,
kusimamishwa kwanza mashambulizi ya jeshi la Syria. Pamoja na hayo,
mafanikio kidogo sana yalifikiwa hasa juu ya kuanza vikao vya wataalamu
baina ya Umoja wa Mataifa na upande wa Syria katika uwanja wa
kujadili katiba na masuala mengine ya kisheria ambayo yalisisitizwa pia
na Staffan de Mistura. Ama suala jingine ni kwamba, kiwango cha maudhui
ambazo zilitakiwa kujadiliwa katika mazungumzo ya Geneva sita zilikuwa
nyingi.
Kwa mfano mwingine ni kwamba, suala la
katiba ni lenye umuhimu mwingi ambapo kila upande linaupa mazingatio
maalumu. Kiujumla ni kwamba kuhusiana na katiba kuna njia tatu ambazo ni
kuifanyia marekebisho, kuisimamisha na kuibadilisha, suala ambalo bila
shaka pande zote zina msimamo unaotofautiana. Na ili kufikiwa
makubaliano kuhusiana na masuala hayo kutahitajia muda mwingi zaidi. Kwa
ibara nyingine ni kwamba, kila suala lenye taathira ya mazungumzo
katika kugawana madaraka, ndivyo ambavyo huwa na umuhimu zaidi huku njia
za kufikiwa makubaliano juu yake zikiwa ngumu vile vile.
Nukta nyingine ni hii kwamba, kivuli cha
upande wa Marekani katika kukwamisha mazungumzo kuhusiana na mgogoro wa
Syria, bado kinaendelea kushuhudiwa katika mwenendo huo. Kuhusiana na
hilo, ni kwamba katika hali ambayo ujumbe unaoiwakilisha serikali ya
Damascus na makundi ya upinzani chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa
yalikuwa yakiendelea na mazungumzo yao ya mjini Geneva, ndege za
muungano unaoongozwa na Marekani, zilishambulia msafara wa kijeshi wa
serikali ya Syria, kitendo ambacho kilitajwa na Bashar Jaafar,
mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa kuwa ni aina ya ugaidi wa
kimataifa.
Ukweli ni kwamba, kwa upande mmoja
Marekani ilitekeleza kitendo hicho cha kijeshi na kilicho kinyume na
sheria ili kuyapa matumaini makundi ya kigaidi kwamba, Washington bado
inayaunga mkono magenge hayo na kwamba yasiwe na wasi wasi wowote juu ya
kuvunjika mazungumzo hayo. Na kwa upande mwingine ni kwamba, hujuma
hiyo ilisaidia kufelisha mazungumzo yanayoendelea kuhusiana na mgogoro
wa taifa hilo la Kiarabu. Hata hivyo na licha ya matatizo yote hayo, na
kwa mujibu wa pendekezo la Staffan de Mistura, mjumbe wa Umoja wa
Mataifa katika masuala ya Syria, imepangwa kufanyika mazungumzo ya
Geneva saba kuhusiana na mgogoro wa nchi hiyo katikati ya mwezi Juni
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment