Roger Moore nyota wa filamu alieigiza kwa muda mrefu zaidi kama James Bond, amefariki nchini Uswisi kwa maradhi ya Saratani akiwa na miaka 89.
Roger Moore hakuwa mtu aliejigamba kuhusu uwezo wake wa kuigiza lakini ukweli ulijidhihirisha wenyewe -- aliigiza kama James Bond katika filamu nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Akijulikana kwa nyusi zake zilizopanda juu kiajabu na stihizai zisizoonyesha hisia, mtazamano wa Moore kuhusu jasusi huyo wa juu alikuwa mcheshi zaidi kuliko mtangulizi wake Sean Conery.
Lakini alimpiku Conery na waigizaji wote waliowahi kuigiza 007 kwa kuigiza nafasi aliopendelea kuiita "Jimmy Bond" katika rekodi ya filamu saba. Moore pia alikuwa wa mwisho miongoni mwa nyota wa filamu wa mfumo wa kizamani, aliewahesabu Frank Sinatra na David Niven miongoni mwa marafiki zake na aliishi maisha ya anasa nchini Uswisi na kwenye pwani ya Meditrannia ya kusini-masahriki mwa Ufaransa.
Aliendelea kuwa shujaa wa maisha halisi na balozi wa shirika la UNICEF hata wakati akipuuza vipaji vya mwenyewe. "Mimi siyo aina ya muuaji ya kinyama. Ndiyo maanda naigiza nafasi hiyo zaidi kwa kuchekesha," aliwahi kunukuliwa akisema.
Roger Moore katika filamu ya "Moonraker" akiwa na Lois Chiles alieigiza kama Holly Goodhead na Richard Kiel alieigiza kama Jaws.
Mwanzo wa kazi ya uigizaji
Roger George Moore alizaliwa Oktoba 14, 1927 katikakiunga cha jiji la London cha Stockwell, akiwa mtoto pekee wa afisa wa polisi mwenye cheo cha constable na mke wake, na alikulia katika maisha mazuri. " Sikuwa na maisha mabaya kama mvulana kutoka Stockwell, ambako nilikuwa naangalia cinema kwa mshangao, bila kujua kwamba ningekuwa sehemu ya ulimwengu huu wa ajabu," aliandika katika wasifu wake," Uliwengu wangu ni Bond wangu."
Moore alianza kazi ya uingizaji kama msaidizi katika miaka ya 1940 kabla ya kusoma katika chuo cha kifalme cha masomo ya sanaa ya maigizo. Alipata mkataba wa studio za MGM lakini alikuwa tu na jukumu la usaidizi katika miaka 1950. Ilikuwa ni katik muongo uliofuata ambapo alipata umaarufu duniani, akiigiza katika kipindi cha televisheni cha Uingereza "The Saint" kama Simon Templer, mpenda vituko mwenye kujisifu.
Moore alisema katika wasifu wake kwamba aliwahi kuombwa kuigiza James Bond mwaka 1967. Lakini ilikuwa mwaka 1973 ambapo alipata nafasi hiyo -- licha ya kuwa kwa umri wa miaka 45, alikuwa mkubwa kwa mwaka mmoja na nusu zaidi yaConnery, mtu aliemrithi katika nafasi hiyo.
Roger katika kipande cha filamu ya "View to a Kill" ya mwaka 1985 akiwa na "Bond Girl" Tanya Roberts.
Moore aliigiza mara ya kwanza katika filamu ya "Live and Let Live", baaday a watengenezaji kumfanya aüunguze uzito, kuwa fiti na kukata nywele zake. Alifuatia filamu hiyo na "The Man With the Golden Gun" (1974), "The Spy Who Loved Me" (1977), "Moonraker" (1979), "For Your Eyes Only" (1981) na "Octopussy" (1983) kabla ya kutupa daruga baada ya kuigiza "A View to a Kill" mwaka 1985, akiwa na umri wa miaka 57.
Moore alisema filamu ya Bond alioifurahia zaidi ni "The Spy Who Loved Me", inayokumbukwa kwa kuhusisha nafasi kadhaa za uhalifu zilizohusisha mfano "Jaws" ilioigizwa na Richard Kiel -- aliefariki 2014, na vifaa vikiwemo gari la mashindano la Lotus Esprit, ambalo lilitumika vilevile kama nyambizi.
"Nadhani 'The Spy Who Loved Me' ndiyo ilikuwa bora, au kwa meneno mengine nilioifurahia zaidi," Moore aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP katika mahojiano kwa njia ya barua pepe mwaka 2007. "Ilikuwa na maeneo mazuri. Na nilifurahia kupita kiasi kufanya kazi na mkurugenzi Lewis Gilbert.
Moore aliigiza katika filamu nyingine wakati na baada ya miaka ya Bond lakini hakuna kati ya hizo filamu nyingine iliokuwa na mafanikio kama ya 007. Moore pia alifurahi maisha ya hali ya juu, akiwa na kundi la nyota na majumba kusinimagharibi mwa Uswisi na Monaco.
Balozi wa hisani wa UNICEF
Lakini katika miaka ya karibuni Moore alijulikana kwa kazi zake za kiutu, kupitia shughuli kama balozi wa hisani wa UNICEF, akisaidia kukusanya feza kwa ajili ya watoto wanaoishi katika maisha magumu. Alipewa hadhi ya shujaa wa ukoo bora mwaka 2003 katika kutambua kazi yake na shirika hilo.
Roger Moore alivyoonekana katika picha hii iliochukuliwa 25.06.2013 kabla ya kufanyiwa mahojiano mjini Aachen, na shirika la habari la Ujerumani dpa.
Mwaka 1993 alifanyiwa upasuaji wa saratani ya tezi dume, mwaka 2003 aliwekewa kifaa cha mapigo ya moyo "pacemaker" na 2013 aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa kisukari. Mwaka 2014 alichapisha kitabu chake cha "Last Man Standing: Tales from Tinseltown" kilichopewa kichwa cha "One Lucky Bastard" nchini Marekani. Mwaka 2015 alishika nambari 38 katika jarida la Uingereza la GQ miongoni mwa wanaume wanaopendeza zaidi kimavazi.
Moore aliowa mara nne na ameacha watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike. Watoto wake wote aliwazaa na muigizaji wa Kitaliano Luisa Mattioli, aliemuoa mwaka 1969 na kumtaliki 1996. Kisha alimuoa Msweden Kristina Tholstrup mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment