Viongozi wa serikali ya Côte d’Ivoire wametangaza kufikiwa makubaliano na askari waasi wa nchi hiyo.
Alain Richard Donwahi, Waziri wa
Ulinzi wa Côte d’Ivoire amesema kuwa, tayari yamefikiwa makubaliano na
askari hao waasi nchini. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa askari
hao wametangaza habari ya kutofikiwa makubaliano na serikali ya taifa
hilo Uasi wa askari nchini Côte d’Ivoire uliibuka siku ya Jumapili
iliyopita kwa kufanya vurugu katika mji wa kibiashara wa Abidjan
na Bouaké.
Mapema jana watu sita waliripotiwa kujeruhiwa kwa risasi huko Bouaké,
ambao bado uko mikononi mwa wanajeshi hao walioasi nchini
Kodivaa. Shirika la habari la Ufaransa liliripoti kuwa, wanajeshi waasi
waliwafyatulia risasi watu katika mji wa pili wa Ivory Coast ulioko
mikononi mwa wanajeshi hao waaasi katikati ya nchi hiyo ya magharibi mwa
Afrika. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mwanamke mmoja na wanaume watano
wamejeruhiwa kwa risasi na kuwahishwa hospitalini huko Bouaké.
Kabla ya hapo pia, Baraza la Usalama wa Taifa la Ivory Coast
lilifanya kikao cha dharura kufuatia kushadidi fujo zilizosababishwa na
uasi huo wa wanajeshi.
No comments:
Post a Comment