Vyombo vya habari nchini Iran vinaendeshwa na serikali
au vinadhibitiwa sana. Lakini kabla ya uchaguzi wa rais, watu wana uhuru
wa kujieleza katika mitandao ya kijamii hata kama ni kidogo.
Matumizi ya mitandao ya kijamii Iran
Rais wa Iran Hassan Rohani
Iran
itachaguwa rais wake mpya hapo kesho Ijumaa tarehe 19 mwezi wa Mei, na
hali katika mitandao ya kijamii inazidi kupamba moto. Kama ilivyo
kawaida ya nchi nyingi ambazo zinadhibiti utumiaji wa mitandao ya
kijamii na vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, Iran sasa imepata uhuru
wa muda mfupi wa kujieleza. Juu ya yote, watumiaji wa mitandao ya
kijamii wanachukua nafasi hiyo kuelezea mawazo yao, na mahitaji juu kwa
wagombea.
Wanasiasa pia wanatumia mitandao ya kijamii kama njia
ya kuhamasisha wapiga kura. Mapema Mwezi huu wa Mei, Kiongozi mkuu wa
kidini Khamenei, mtumiaji wa mara kwa mara wa Twitter, alitoa wito kwa
Wairani wote kutumia haki yao ya kupiga kura. Khamenei alisisitiza
kwamba wapigakura wajitokeze tarehe 19 Mei ili wathibitishe mfumo wa
kisiasa wa Iran.
Khamenei aliandika ifuatavyo katika mtandao wake
wa twitter: Jamhuri ya kiislamu msingi wake ni kura ya watu. Uislamu
unatuambia tufuate njia ya watu kupiga kura.
Hamu kwa ajili ya elimu ya siasa
Kipindi
kabla cha uchaguzi kinatoa fursa kuu kwa wanaharakati mtandaoni
kugundua unyanyasaji na kutekeleza malengo ya muda mrefu.
"Tunaona
kuwepo kwa hamu kubwa juu ya elimu ya siasa. Na huo ndio mwenendo
unaoonekana katika mitandao ya kijamii," mwanaharakati wa haki za
binadamu na muandishi wa habari Reza Haghighatnejad aliliambia shirika
la habari la Deutsche Welle.
Reza Haghighatnejad mwanaharakati na muandishi wa habari nchi Iran
Mwanaharakati huyo amekuwa akichunguza shughuli za mitandao ya jamii za Wairan na matumizi yao ya mtandao.
"Wengi
wao wanataka kuburudishwa. Ukweli ni wengi wao hawana mvuto hasa katika
maswala ya siasa. Lakini kinachotupa tamaa ni uongezekaji wa watumizi
wa mtandao kushiriki katika kampeni wakiwa na malengo ya muda mrefu,"
alisema Reza.
Maslahi ya ghafla katika haki za wanawake
Masuala
kama hayo ya kijamii sio tu kupokea msaada mpana katika mitandao ya
kijamii, lakini pia wanawake wamekuwa mandhari ya kampeni kwa wagombea
wa urais.
" Tunawaona wagombea wa uraisi ghafla wametambua
umuhimu wa haki za wanawake na masuala ya haki za raia. Ni wakati wa
kupaza sauti ambao unaweza kukufanya wewe ukaamini kuwa wako na
wapinzani," alisema mchunguzi wa mambo ya jinsi katika chuo kikuu cha
Toronto Victoria Tahmasebi-Birgani."
Birgani amesema kuwa
wagombea wote ni wanachama wa mfuno wa siasa wa nchi hiyo, na mfumo huo
unawakilisha wanaharakati wa haki za wanawake. Lakini pia mitandao ya
kijamii imefanya kuwa haiwezekani kutogusia suala la uhuru na usawa wa
jamii.
Wanawake wa Iran katika upigaji kura 2013
Iran
ni nchi yenye vijana wengi,na wengi wakiwa katika rika la miaka 30.
Asilimia 80 ya wairain wanaweza kusoma na kuandika. Iran inatilia sana
umuhimu wa elimu, lakini elimu ya siasa nikama haipo mashuleni na katika
vyuo vikuu. Vyombo vya habari ni vya serikali au vinadhibitiwa vikali.
"Kituo
cha radio na televisheni cha IRIB cha Iran ni vya serikali na
vinadhibitiwa na wahafidhina. ripoti nyingi ni za upande mmoja na
zinathibisha mpango wa wahafidhina," msomi wa sayansi ya siasa Sadegh
Zibakalam aliliambia shirika la habari la Deutsche Welle.
Harakati za mitandaoni zinachukuliwa kuwa kama makosa ya mitandaoni
Chini
ya Uongozi wa rais wa sasa Hassan Rouhani, na hasa katika kufuatilia
kukamilika kwa mpango wa ufanisi wa nyuklia, nchi hiyo pole pole imeanza
kufunguka. katika kufunguka huku Iran na ubadilishanaji na ulimwengu
wa nje ya Iran imeimarisha jamii ya umma na kazi zake ya elimu ya
mtandaoni.
"Lakini sehemu chache tu ndio zinaonekana
kupata faida mpaka sasa. Sehemu hizi ni zile ambazo haziwi na migogoro
ya moja kwa moja na dhana ya maadili ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,"
alisema muandishi wa habari Reza Haghighatnejad.
"Serikali imeona
nguvu ya mitandao ya kijamii. Wanachama wake wote wanatumia mitandao
hiyo, kutoka mkuu wa kiongozi hadi wagombea urais," anasema
Haghighatnejad.
Muandishi huyu wa habari alisema pia kuwa
wanasiasa hao wanatumia mitandao kusambaza malengo yao ya kisiasa,
lakini bado wanapinga upatikanaji kamili wa utumiajiwa mitandao kwa watu
wote.
" Hata hivyo, wamepoteza udhibiti wao taarifa," alisema muandishi wa habari na mwanaharakati Reza Haghighatnejat.
No comments:
Post a Comment