Korea Kaskazini imelaani tena jaribio la
kutaka kumuua kiongozi wake ambalo limetekelezwa mashirika ya kijasusi
ya Marekani na Korea Kusini na kulitaja jaribio hilo kuwa sawa na
tangazo la vita.
Katika taarifa, Ubalozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa
Mataifa umetoa taarifa na kusema nchi yake itaanza oparesheni dhidi ya
magaidi ambao walihusika na njama ya kutoka kumuua kiongozi wa nchi hiyo
Kim Jong-un.
Taarifa hiyo imesema Pyongyang ina azma imara ya kuwasaka bila huruma
na kuwaangamiza magaidi wote wa shirika kuu la kijasusi la Marekani CIA
na shirika la kijasusi la Korea Kusini waliohusika na njama hiyo.
Taarifa hiyo imetoa wito kwa nchi za Umoja wa Mataifa kuunga mkono
jitahada za Korea Kaskazini katika kukabiliana na magaidi hao waliotumwa
na CIA.
Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilitoa taarifa na kusema kuwa, CIA na
Idara ya Intelijensia ya Korea Kusini zinapanga kutumia silaha ya
kemikali kumuua kiongozi wa nchi hiyo.
Haya yanajiri katika hali ambayo, hali ya taharuki ingali imetanda
katika Peninsula ya Korea haswa baada ya Marekani kufanyia majaribio
kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu
kilomita elfu sita na 760.
No comments:
Post a Comment