Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon
imeitaja safari ya Rais Donald Trump wa Marekani nchini Saudi Arabia
kama ya kiwendawazimu na ambayo haitakuwa na tija yoyote kwa ulimwengu
wa Kiislamu.
Sayyid Hashem Saifuddin, Rais wa Baraza Kuu la Hizbullah
amesema Washington haina uwezo wa kudhuru au kuweka kizingiti kwenye
shughuli za harakati hiyo ya muqawama.
Amesema safari ya Trump nchini Saudia ni ithibati kuwa Hizbullah
inazidi kupata nguvu kila uchao kiasi cha kuwakosesha usungizi na
kuwatia kiwewe maadui wa muqawama.
Amesema: "Malengo ya utawala wa kiwendawazimu wa Washington chini ya
Trump hayatafikiwa katika safari hiyo ghairi ya kupata kuangaziwa tu na
vyombo vya habari."
Hii ni katika hali ambayo, Ijumaa iliyopita, utawala wa Riyadh
ulitangaza kumuwekea vikwazo afisa huyo wa ngazi za juu wa Hizbullah ya
Lebanon. Itakumbukwa kuwa, mwezi Februari mwaka huu, Katibu Mkuu wa
Hizbullah, Sayyid Hassan Nasrullah alisema Trump ni mtu mpumbavu.
Hivi karibuni, kikao cha siri cha upangaji njama dhidi ya harakati ya
Hizbullah kilifanyika mjini Washington, Marekani na kuhudhuriwa na nchi
za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi PGCC.
No comments:
Post a Comment