Asilimia takriban 63.5 ya
walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na Kituo cha
Utafiti cha Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran IRIB wameamua kuwa watashiriki katika uchaguzi huo unaotarajiwa
kufanyika tarehe 19 mwezi huu wa Mei na asilimia 7.1 wengine wamesema
huenda wakashiriki kwenye uchaguzi huo.
Uchunguzi huo wa maoni umefanyika kwa
kuwauliza maswali watu 38,000 walio na umri wa zaidi ya miaka 18 katika
mji mkuu Tehran na katika miji mikuu ya mikoa ya Iran na pia katika miji
mingine miwili yenye watu wengi pamoja na vijiji 10 kutoka katika kila
mkoa wa Iran. Uchunguzi huo ulianza siku ya Jumapili na kumalizika juzi
Jumanne (kuanzia Aprili 30 hadi Mei 2).
Asilimia takriban 23.6 ya waliojibu
maswali waliyoulizwa wameamua hawatoshiriki na asilimia 1.2 wengine
wamesema huenda wasishiriki. Asilmia 4.6 wengine wamesema hawajaamua
iwapo watashiriki katika kupiga kura au la.
Uchunguzi huo wa maoni umefanyika baada
ya mjadala uliorushwa hewani mubashara kati ya wagombea sita wa urais,
Ijumaa iliyopita na unaonesha kuongezeka idadi ya watu walioamua
kushiriki kwenye uchaguzi baada ya mjadala huo.
Uchunguzi mwingine wa maoni uliofanywa
na shirika la IRIB kabla ya mjadala huo ulikuwa umeonesha kuwa, asilmia
56.1 tu ya wapiga kura ndio waliokuwa na nia ya kushiriki kwenye
uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment