Maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini
wanaendelea kumiminika nchi jirani ya Sudan wakitafuta mahala salama
katika nchi ambayo walijitenga nayo miaka kadhaa iliyopita.
Sudan Kusini ilijitenga na Sudan mwaka 2011 kwa kupiga kura ya
maoni iliyoungwa mkono na asilimia 99 ya raia wake baada ya vita vya
miongo kadhaa vya kutaka uhuru. Inasadikiwa kuwa Sudan Kusini
ilichochewa na madola ya kibeberu kujitenga na Sudan.
Zaidi ya raia 375,00 wa Sudan Kusini, aslimi 90 wakiwa ni wanawake na
watoto, wamekimbia Sudan tokea vita vya ndani vianze katika nchi yao
mwaka 2013. Uganda nayo ina wakimbizi 883,000 kutoka Sudan Kusini huku
wengine wakikimbilia nchi jirani ya Kenya.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limesema
idadi ya Wasudan Kusini wanaokimbilia Sudan inazidi kuongezeka. UNCHR
imesema mwezi uliopita pekee raia 23,000 wa Sudan Kusini waliingia
Sudan na kwa ujumla mwaka huu idadi hiyo ni 108,000. Imetabiriwa kuwa
mwezi ujao raia wengine 50,000 wa Sudan Kusini watakimbilia Sudan
wakitoroka vita na njaa katika nchi yao.
Vita vya ndani nchini humo vilivyoanza Disemba 2013 vimesababisha
mauaji ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa
wakimbizi. Nchi hiyo, ambayo ilijitenga na Sudan mwaka 2011, ilitumbukia
katika vita vya ndani baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka
kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba
alihusika na jaribio la kupindua serikali yake.
No comments:
Post a Comment