Chama cha Christian Demokrat (CDU) cha Kansela Angela
Merkel wa Ujerumani kimekipita sana chama cha mrengo wa kati kulia cha
Social Demokrat (SPD) katika uchaguzi wa jimbo la kusini magharibi la
Saarland.
.
Katika uchaguzi uliofanyika Jumapili (26.03.2016)Chama cha CDU
kimeshinda kwa asilimia 40.4 wakati chama cha SPD kimejipatia asilimia
30.4 na hiyo kuvunja matumaini kwamba kingeliweza kuendeleza msukumo
wake baada ya kuwasili kwa spika wa zamani wa bunge la Ulaya Martin
Schulz kuchukuwa uongozi wa chama hicho.
Baada ya miaka mingi ya
kutofanya vizuri chama hicho cha SPD kilijiongezea pointi 10 kulingana
na uchunguzi wa maoni baada ya Schulz kutangaza kwamba atagombea
kumn'gatuwa Merkel katika uchaguzi mkuu wa tarehe 24 mwezi wa Septemba
kwa kile inachotajwa kama "taathira ya Schulz."
Makadirio ya ZDF
yanaonyesha kwamba cha sera kali za mrengo wa kulia AfD ambacho kina
kama asilimia 9 katika ngazi ya taifa,mzozo wa wakimbizi wa Ulaya ambao
unechochea kuungwa mkono kwa chama hicho mwaka jana umepunguwa na chama
hicho kimezongwa na mfarakano wa ndani ya chama
AfD yajivunia matokeo
.
Martin Schulz akizungumzia matokeo ya uchaguzi wa Saarland.
Mkuu
wa chama hicho Mbadala kwa Ujerumani Bibi.Frauke Petry amesema
anajivunia matokeo ya chama chake lakini ameelezea kuvunjika moyo na
uamuzi wa wapiga kura kuchaguwa kuendelea na muungano mkuu wa chama cha
CDU na SPD kuliongoza jimbo hilo.
Chama cha sera za mrengo wa
kushoto Di Linke cha jimbo hilo la Saarland chini ya waziri wa zamani wa
fedha mwenye ushawishi mkubwa Oskar Lafontaine kimejipatia asilimia
14.4 ya kura na kukifanya kuwa chama cha tatu chenye nguvu kubwa katika
jimbo hilo.
Wakati huo huo chama cha Kijani cha mazingira na kile
chenye kupendelea biashara cha FDP vimepata pungufu ya asilimia tano
kiwango kinachohitajika kuweza kurdi tena katika bunge la jimbo kwa
mujibu wa makadirio hayo ya kituo cha matangazo cha ZDF.
Merkel anautaka muhula wa nne
Matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Saarland.
Merkel
ambaye amekuwa akiongoza serikali mara tatu mfululizo tokea mwaka 2005
anataka kuwania muhula wa nne katika uchaguzi wa Septemba na uchaguzi
huo wa jimbo la Saarland ulikuwa ukiangaliwa kama mtihani wake wa kwanza
kwa nafasi alio nayo wakati wa uchaguzi mkuu.
Kansela amekuja
kushutumiwa nchini kwa uamuzi wake wa kuwafungulia mipaka mamia kwa
maelfu ya wahamiaj hapo mwaka 2015 .Pia amekuwa akituhumiwa kukisukuma
chama chake mrengo wa kushoto na kuzijumuisha baadhi ya sera za chama
cha SPD na hiyo kuchochea kuibuka kwa chama cha AfD.
No comments:
Post a Comment