Wanajeshi wa Misri katika operesheni ya kupambana na mgaidi, Sinai Kaskazini
Jeshi la Misri leo limetoa taarifa na kusema
kuwa, limefanikiwa kuua magaidi watano na kuwatia mbaroni wengine 16
katika operesheni maalumu iliyofanywa na jeshi hilo kaskazini mwa Misri.
Msemaji wa jeshi la Misri, Kanali
Tamer el Refae amesema, magaidi watano wakufurishaji akiwem mmoja wa
viongozi wa kundi la kigaidi Baytul Muqaddas linalofanya mashambulizi
yake mengi kaskazini mwa Rasi ya Sinai wameuawa kwenye operesheni hiyo.
Amesema, magaidi wengine 16 wametiwa mbaroni katika opereseheni hiyo.
Kwa mujibu wa Kanali Tamer el Refae,
jeshi la Misri limekamata pia kiwango kikubwa cha silaha pamoja na
kutegua mabomu yaliyokuwa yametegwa na wanamgambo hao.
Eneo la Sinai Kaskazini huko Misri
limeshuhudia mashambulizi mengi ya kigaidi tangu mwaka 2013 baada ya
jeshi la nchi hiyo kufanya mapinduzi yaliyoongozwa na Rais wa hivi sasa
wa Misri, Jenerali Abdul Fattah el Sisi. Mapinduzi hayo ya kijeshi
yalimuondoa marakani rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini
Misri, Mohammad Morsi ambaye hivi sasa yuko jela. Al Arish ambayo ndiyo
makao makuu ya mkoa huo wa kaskazini mwa Misri ndio mji unaoshuhudia
mashambulizi mengi ya kigaidi.
Hadi hivi sasa kundi la Ansar Baytul
Muqaddas limeshafanya makumi ya mashambulizi dhidi ya maeneo ya
wanajeshi na raia wa kawaida wa Misri na kuua watu wengi sambamba na
kuharibu miundombinu ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
No comments:
Post a Comment