Afisa wa ngazi za juu nchini Iran amesema
kuwa, hujuma za ndege za kivita za Marekani katika mji wa Mosul, Iraq
ambazo zimeua idadi kubwa ya raia, ni jinai za kivita.
Ali
Shamkhani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema,
jinai iliyofanywa na Marekani huko Mosul ni sawa na jinai za kivita
zinazofanywa na magaidi wa Daesh (ISIS) pamoja na makundi mengine ya
magaidi wakufurishaji ambao wanawalenga raia na watu wasio na hatia.
Amesema jinai hizo za Marekani zinapaswa kushughulikiwa haraka
iwezekanavyo katika mahakama ya kimataifa.
Siku
ya Jumamosi Marekani ilikiri ilifanya mashambulizi ya angani huko
magharibi mwa Mosul mnamo Machi 17 mwaka huu na kuua raia 200. Wakuu wa
Iraq wanasema Mareknai ilifanya hujuma kadhaa siku hiyo.
Shamkhani amesema, hata kama Marekani
inadai eti hujuma hiyo haikuwa ya makusudi, lakini hilo haliwaondoi
hatiani Wamarekani waliotenda jinai hiyo. Shamkhani amesema, jeshi la
Marekani limekuwa likiua raia wasio na hatia katika eneo hili kwa
kisingizo cha kupambana na ugaidi.
Umoja
wa Mataifa pia umetangaza kushtushwa na kupoteza maisha raia katika
shambulio hilo la Marekani mjini Mosul, kaskazini mwa Iraq.
No comments:
Post a Comment