Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran katika Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amesema
silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni wa Israel ni tishio kwa amani
na usalama wa kimataifa na ametaka wakala huo uchunguze na kufuatilia
kwa uzito mkubwa mpango wa silaha za nyuklia wa utawala huo.
Reza Najafi ametoa wito huo jana katika siku ya mwisho ya kikao
cha msimu cha Bodi ya Magavana wa IAEA, ambapo mbali na kuashiria jinsi
nchi wanachama wa Harakati Isiyofungamana na Siasa za Upande Wowote
(NAM) zilivyolaani vikali mpango wa silaha za nyuklia wa utawala wa
Kizayuni, ametaka suala hilo lizingatiwe kwa makini na kufuatiliwa kwa
uzito mkubwa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.
Najafi ameashiria wito uliotolewa mara kadhaa na jamii ya kimataifa
kupitia maazimio ya IAEA na mikutano ya kuangalia upya Mkataba wa Kuzuia
Uundaji na Uenezaji Silaha za Nyuklia (NPT) wa kuutaka utawala haramu
wa Israel ujiunge haraka na mkataba huo na kuweka vinu vyake vya nyuklia
chini ya usimamizi na uangalizi kamili wa IAEA na kueleza kuwa, kwa
masikitiko, katika miaka yote hii utawala wa Kizayuni, kwa kupuuza wito
wa kisheria wa jamii ya kimataifa na kwa uungaji mkono kibubusa wa
baadhi ya nchi za Magharibi umeendelea kukiuka waziwazi sheria na
kaununi zote za kimataifa na kuendeleza mipango yake ya kijeshi ya
nyuklia.
Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Wakala wa
Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) amekosoa vikali pia tabia ya
kindumakuwili ya baadhi ya nchi za Magharibi kuhusiana na kuzuia ueneaji
wa silaha za nyuklia na katika kutekeleza marufuku kamili ya kutoipatia
Israel zana na mada za nyuklia, utawala ambao kutokana na historia yake
iliyojaa vitendo vya uvamizi, ukaliaji ardhi kwa mabavu na ugaidi wa
kiserikali, ni tishio kwa amani na usalama wa dunia.../
No comments:
Post a Comment