Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, March 4, 2017

JENGO LA REDIO YA GENGE LA DAESH, MOSUL LADHIBITIWA NA JESHI LA IRAQ

Habari kutoka mkoa wa Nainawa (Nineveh) nchini Iraq zinaarifu kwamba jeshi la nchi hiyo limedhibiti jengo la redio ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh kwa jina la al-Bayan.
Jeshi la Iraq limekomboa eneo la Jawasaq katika pwani ya upande wa kulia ya mji wa Mosul, sambamba na kubaini jengo na mnara wa kurushia matangazo wa redio ya kundi hilo kwa jina la al-Bayan katika mji huo. Kabla ya jeshi la Iraq kuwasili katika eneo hilo, genge hilo la kigaidi lililichoma moto jengo la redio hiyo ili kupoteza ushahidi.
Gaidi wa Daesh akiwa redioni zamani
Hata hivyo jeshi la Iraq liliweza kunasa nyaraka muhimu katika nyumba iliyokuwa karibu na jengo la redio hiyo ambazo zinajumuisha ripoti muhimu za kiintelijensia za timu yote ya kundi hilo.
Itafahamika kuwa, redio hiyo ya kundi la Daesh (ISIS) ilikuwa ikitangaza kwa lugha tano tofauti na kutoa matangazo ya kuwataka raia kutekeleza operesheni za kigaidi. Kusambaratishwa redio hiyo kunatajwa kuwa pigo jingine kubwa dhidi ya genge hilo linalopata himaya kutoka Marekani, Israel, Saudia na baadhi ya za Kiarabu na Magharibi.
Redio Bayan ya magaidi wa Daesh
Wakati huo huo kitengo cha intelijensia katika jeshi la Iraq kimetangaza habari ya kuuawa Abu Abdur-Rahman al-Answar, kiongozi wa genge la kigaidi kwa jina la Jundul-Khilafah lenye mafungamano na kundi la Daesh huko magharibi mwa mji wa Mosul. Kwa mujibu wa ripoti hiyo gaidi huyo mwenye uraia wa Saudia ameuawa katika shambulio la anga akiwa pamoja na viongozi wengine sita wa kundi hilo.
Jengo hilo baada ya magaidi hao kuliteketeza moto
Jeshi la Iraq lilmetanga kuwa, kundi  la Daesh (ISIS) limekuwa likitumia silaha zenye gesi ya sumu katika kulizuia jeshi hilo kusonga mbele katika maeneo yaliyosalia ya mji huo wa Mosul.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages