Kwa akali watoto milioni 1.7 wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na kuvuta hewa chafu kote duniani.
Ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani (WHO) imefafanua kuwa,
kiwango hicho ni sawa na asilimia 25 ya vifo vya watoto wadogo walio na
umri wa chini ya miaka mitano kote duniani.
WHO imebainisha kuwa, mazingira machafu, hewa na maji machafu pamoja
na moshi wa sigara yanasababisha robo ya vifo vya watoto wadogo kote
duniani kila mwaka.
Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema
kuwa, hewa na maji machafu yamechangia watoto wengi kupatwa na maradhi
ya pumu, malaria, kutapika na kuendesha, magonjwa ambayo yanaongoza kwa
vifo vya watoto wadogo duniani.
Mwaka jana 2016, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilionya kuwa hali ya
uchafuzi wa hewa inazidi kuwa mbaya duniani kote huku zaidi ya asilimia
80 ya wakaazi wa miji mikubwa wakivuta hewa chafu na kuongeza hatari ya
kupatwa na saratani ya mapafu na maradhi mengine hatari.
No comments:
Post a Comment