Maelfu ya raia wa Syria wameyakimbia mapigano makali
kati ya vikosi vya serikali vinayoungwa mkono na Russia na wapiganaji
wa jihadi wa kundi lilalojiita Dola la Kiislamu wiki moja iliopita.
Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa na mashambulizi ya anga na
mizinga ya Russia vimeendesha mapambano makali dhidi ya kundi la Dola la
Kiislamu na kuviteka takriban vijiji 80 viliokuwa kwenye mikono ya
wapiganaji hao wa jihadi tokea katikati ya mwezi wa Januari.
Kwa
mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria lengo
la mashambulizi ya vikosi vya serikali ni kuuteka mji wa Kahafsah
unaoshikiliwa na kundi la IS mji ambao una kituo kikuu chenye kusambaza
maji kwa mji wa Allepo.
Wakaazi katika mji wa Allepo ambao ni mji
wa pili kwa ukubwa nchini Syria wamekuwa hawapati huduma ya maji kwa
siku 47 baada ya wapiganaji wa jihadi kukata usambazaji wa maji kwa mji
huo.Mapigano hayo katika kipindi cha wiki moja yamesababisha wimbi la
zaidi ya raia 30,000 kukimbia wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Wengi wakimbilia mji wa Manbij
Miji ya Syria yageuzwa magofu kutokana na mapigano.
Mkuu
wa shirika hilo Rami Abdel-Rahman amesema wengi ya watu waliokimbia
mapigano hayo wamekwenda kwenye maeneo karibu na mji wa Manbij
unaodhibitiwa na vijkosi vya (SDF) washirika wa wapiganaji wa Kikudi na
Waarabu wanaoungwa mkono na Marekani ambayo pia inapambana na kundi hilo
la IS.
Wengi wao wameshuhudiwa wakielekea katika mji huo kwa
kutumia piki piki,mabasi madogo na magari na wengi wao wameonekana kuwa
wachovu wakiwa katika misururu kwenye kituo cha ukaguzi kwa jili ya
kupekuliwa na kupata ruhusa ya kuingia.
Ibrahim al-Quftan
mwenyekiti mwenza wa mamlaka ya kiraia ya mji wa Manbij ameliambia
shirika la habari la AFP kwamba takriban watu 40,000 wamewasili katika
mji huo katika siku za hivi karibuni.Ameongeza kusema idadi hiyo ya watu
waliopotezewa makaazi inaendelea kuongezeka kutokana na mapigano kati
ya majeshi ya serikali ya Syria na kundi la Daesh kama
linavyotambulikana kwa Kiarabu (Dola la Kiislam).
Mji waemewa na wimbi jipya la waliopoteza makaazi
Wanajeshi wa Russia wakishiriki mapigano katika mji wa Allepo.
Na
kwa mujibu wa Abdel Rahman wa shirika la haki za binaadamu nchini Syria
mji huo wa Manbij tayari unawapa hifadhi maelfu ya watu waliopotezewa
makaazi ambao waliyakimbia mapigano yaliyopita katika eneo hilo na
wanaishi katika mazingira magumu.Amesema hali hiyo itafanya iwe vigumu
kwa mamlaka ya mji huo kukaribisha wimbi jipya la watu waliopotezewa
makaazi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kushughulikia mahitaji yao ya
msingi.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Syria hapo
mwezi wa Machi mwaka 2011 zaidi ya nusu ya idadi ya watu wake kabla ya
vita hivyo kuanza wamelazimika kuyakimbia makaazi yao.Mkoa wa kaskazini
wa Aleppo una maelfu ya Wasyria waliopotezewa makaazi wengi wao wakiwa
katika makambi na mpaka na Uturuki.
Zaidi ya watu 310,000
wameuwawa tokea mzozo huo wa Syria ulipoanza kwa maandamano ya kupinga
utawala wa Rais Bashar al-Assad lakini juhudi za kimataifa za kukomesha
mzozo hadi sasa zimeshindwa.
No comments:
Post a Comment