Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran, Is'haq Jehangiri
Kufuatia hatua ya Marekani ya kuiwekea Iran
vikwazo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nayo itachukua hatua kadhaa ikiwa
ni pamoja na kuiwekea Marekani vikwazo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran,
Is'haq Jehangiri amesema, serikali ya Iran inachunguza hatua
itakazochukua endapo Marekani itakiuka mapatano ya nyuklia yajulikanayo
kama Mpango wa Pamoja wa Utekeelzwaji JCPOA.
Jehangiri amesema hata kama vikwazo vipya vya Marekani si ukiukwaji wa JCPOA, lakini Marekani itapoteza itibari yake kimataifa.
Jehangiri amesisitiza kuwa, uchumi wa
Iran unazidi kuimarika kutokana na utekelezwaji wa sera za uchumi wa
kimapambano na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa umoja na
mshikamano imeweza kusimama kidete mbele ya vikwazo vikubwa zaidi.
Hivi karibuni wajumbe kadhaa wa vyama
vya Democrat na Republican katika Baraza la Senate la Marekani
walipasisha rasimu ya sheria ya kushadidisha vikwazo dhidi ya Iran.
Kwa mujibu wa rasimu hiyo, watu na
mashirika au taasisi za Iran zitawekewa vikwazo kwa kuhusika na mpango
wa makombora ya kujihami ya nchi hii.
Katika kujibu hatua hiyo, Kamati ya Sera
za Kigeni na Usalama wa Taifa katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu,
Bunge la Iran, linapanga kuwasilisha mswada wa kulitaja Jeshi la
Marekani na Shirika la Kijasusi la Marekani CIA kuwa taasisi za kigaidi.
Aidha katika hatua ya kujibu kufuatia
uhasama na chuki za Baraza la Congress la Marekani, Wizara ya Mambo ya
Nje ya Iran imetangaza kuyawekea vikwazo mashirika 15 ya Marekani
kutokana na mashirika hayo kuunga mkono jinai na ugaidi wa utawala
haramu wa Israel. Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran
imesema mashirika hayo ya Mareknai yamekiuka azimio 2334 la Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuunga mkono ugaidi wa Israel. Aidha
taarifa hio imelaani muswada huo wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
na kuutaja kuwa ni kinyume cha sheria za kimataifa.
No comments:
Post a Comment