António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelitaka
Baraza la Usalama la umoja huo kutuma askari wengine 320 wa kofia buluu
huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
António Guterres alitoa mwito huo
jana Ijumaa kwenye ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
na sambamba na kuelezea kusikitishwa sana na kuongezeka uvunjaji wa
haki za binadamu nchini humo, ametaka kuongezewa nguvu kikosi cha
kimataifa cha kulinda amani MONUSCO ili kiweze kuwa na uwezo mkubwa
zaidi wa kuwalinda raia.
Katika ripoti yake hiyo, Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa aidha ametaka vikosi vingine viwili vitumwe katika miji
ya Lubumbashi na Katanga ili kuzuia miji hiyo kukumbwa na machafuko
wakati wa uchaguzi ujao.
Aidha amesisitiza kuwa, mwaka 2017 ni mwaka muhimu mno kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema, kikosi cha MONUSCO kinafanya
kazi kubwa nchini humo na inabidi kiendelee kuwepo kwa ajili ya
kusimamia mchakato wa kisiasa na kulinda mafanikio yaliyopatikana hadi
hivi sasa katika jitihada za kurejesha amani na utulivu nchini humo.
Kazi kuu ya askari wa Umoja wa Mataifa
nchini Kongo ni kuwalinda raia na wako nchini humo tangu mwaka 1992
chini ya mwavuli wa kikosi cha MONUSCO ambacho hivi sasa kina takriban
wanajeshi 19 elfu wa kofia buluu kutoka nchi mbalimbali duniani.
No comments:
Post a Comment