China imejibu ripoti ya Marekani iliyoituhumu
nchi hiyo kuwa inakiuka haki za na kuitaja Marekani kuwa ndiyo mkiukaji
mkubwa zaidi wa haki za binadamu duniani.
Ripoti iliyotolewa na China imesema hali ya haki za binadamu nchini Marekani inasikitisha mno.
Ijumaa ya jana Baraza la Serikali ya
China lilijibu ripoti ya haki za binadamu iliyotolewa mwaka jana 2016 na
Marekani dhidi yake. Ripoti ya Baraza la Serikali ya Uchina imesema
kuwa, Marekani si tu kwamba haizingatii mipaka ya haki za binadamu ndani
ya nchi, bali hata nje ya nchi hiyo inakanyaga wazi wazi haki hizo.
Hii si mara ya kwanza ambapo Marekani imekuwa ikiandaa ripoti
mbalimbali dhidi ya China ikiituhumu kuwa inakandamiza na kukanyaga haki
za binadamu. Watayarishaji wa ripoti ya Baraza la Serikali ya China
wanasema kuwa, Marekani inashika nafasi ya pili kwenye orodha ya nchi
zinazoongoza kwa kuwa na wafungwa wengi duniani na kila kati ya watu
laki moja wa jamii ya Marekani, 693 wamefungwa jela. Aidha kati ya kila
raia wawili wa Marekani, mmoja wao anamiliki silaha ya moto. Ripoti hiyo
imeeleza kuwa, zaidi ya kesi elfu 58 za hujuma za silaha za moto
zimeripotiwa, ambapo kati ya hizo watu 385 wameuawa kwa silaha hizo.
Ukweli ni kwamba, Marekani hakuna haja ya kurejea kwenye takwimu
zilizotolewa katika ripoti ya Baraza la Serikali ya China ili kutambua
ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanyika nchini humo. Hivi
karibuni Rais wa 45 wa Marekani, Donald Trump ambaye aliyekuwa
akihutubia Bunge la Kongresi la nchi hiyo aliweka wazi uhalisia
uliofichika katika siasa za Marekani. Trump alijikita katika kuzungumzia
migogoro mikubwa ya kijamii, kiuchumi na tofauti kubwa ya kitabaka kati
ya walio nacho na wasiokuwa nacho nchini Marekani na kusema kuwa, uwepo
wa watu milioni 49 wasio na ajira, kusambaratika viwanda elfu 60, uwepo
wa watu milioni 43 wanaosumbuiwa na njaa, kuchaa kwa miundombinu, uwepo
wa magenge ya uhalifu yanayofanya magendo ya dawa za kulevya na
hatimaye kuenea ukatili na chuki nchini humo ni kati ya jinai
zinazoshuhudiwa sana dhidi ya haki za raia.
Uchina kama nchi inayoongozwa na mfumo wa chama kimoja kwa zaidi ya
miongo sita sasa inaonekana katika fikra za walio wengi kama nchi yenye
aina fulani ya udikteta wa kisiasa,. Hata hiyo ukweli ni kwamba, baada
ya Vita vya Pili vya Dunia Marekani iliimarisha nafasi yake kwa kutumia
taasisi kama vile NATO, Benki ya Dunia na Mfumo wa Fedha wa Kimataifa
(IMF). Marekani imezivamia zaidi ya nchi 60 za dunia, kupindu na kuondoa
madarakani makumi ya serikali huru, kuanzisha kambi 800 za kijeshi
katika maeneo mbalimbali ya dunia kwa gharama sawa na asilimia 35 ya
bajeti yote ya kijeshi ya dunia, mambo ambayo yanaidhihirishia dunia
kuwa nchi hiyo ndiye msababishaji wa migogoro ulimwenguni. Jambo lisilo
na shaka ni kuwa Donald Trump hatofautiani na marais waliomtangulia wa
Marekani.
Uchina inaamini kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, Marekani imekuwa
ikipotosha fikra za walio wengi kuhusiana na suala zima la utetezi wa
demokrasia na haki za binaadamu duniani. Uvamizi wa kijeshi wa nchi hiyo
huko Iraq na Afghanistan, unabainisha wazi sera za kindumakuwili na
hadaa nyingi za Washington kwa walimwengu. Kadhalika sera za kuingilia
mambo ya nchi nyingine zinazotekelezwa na Marekani huko katika nchi za
Amerika ya Latini ni kati ya hatua nyingine za watawala wa Washington
kwa lengo la kutaka kuziondoa madarakani serikali huru za mataifa hayo.
Swali la msingi ni kwamba, kwa kuwa na historia hii, Marekani inaweza
kuwa na ustahiki wowote wa kuongoza dunia?
Je kwa mazingira uharibifu mkubwa wa Marekani katika uwanja wa
kukiuka haki za binadamu za mamilioni ya watu duniani wakiwemo hata raia
wake yenyewe, Washington inaweza kuwa mtetezi wa aki hizo na
kuwa mwamuzi na msimamizi wa masuala ya haki za binadamu duniani?
Ni kwa kuzingatia hayo yote ndio maana China ikaitaka Marekani,
badala ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine, ishughulikie
kwanza tatizo la ukosefu makazi la mamilioni ya Wamarekani, kuongezeka
raia wa nchi hiyo wanaokabiliwa na njaa sambamba na kukosa huduma muhimu
za kimaisha. China inaamini kuwa suala la haki za binadamu linatumiwa
na Marekani kama wenzo na fimbo ya kuhalalisha sera za serikali ya
Washington za kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine duniani.
No comments:
Post a Comment