Raia wasiopungua 42 wameuawa katika shambulio
la anga la jeshi la Marekani lililolenga msikiti uliojaa waumini ndani
yake karibu na mji wa Halab (Aleppo) kaskazini mwa Syria. Watu wengine
zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililofanywa katika
kijiji cha al-Jineh kilichopo kilomita 30 magharibi mwa mji wa Halab.
Kwa
mujibu wa ripoti ya kanali ya televisheni ya Press TV shambulio hilo
lililotokea usiku wa kuamkia leo lilifanyika huku watu wapatao 300
wakiwa wamo ndani ya msikiti huo.
Abu
Muhammad, ambaye ni mmoja wa wanakijiji amesema alisikio mlio mkubwa wa
mripuko wakati msikiti huo ulipolengwa, mara baada ya sala ambapo kwa
kawaida hufanyika darsa za wanaume msikitini humo.
Kwa mujibu wa ripoti, watu wengi walikuwa wangali wamekwama ndani ya
msikiti huo ulioporomoka huku waokoaji wakijaribu kuwafukua na kuwatoa
manusura kwenye vifusi.
Katika
taarifa yake, jeshi la Marekani limedai kuwa ndege za kivita za nchi
hiyo ziliwalenga viongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda. Hii ni
katika hali ambayo kwa mujibu wa ripoti, jengo linalodaiwa kufanyika
ndani yake kikao cha wanachama wa kundi hilo la kigaidi lipo umbali wa
mita 15 tu kutoka msikiti ulioshambuliwa na ndege za Marekani.
Kamandi
ya jeshi la Marekani aidha imetangaza kuwa itachunguza ripoti kwamba
katika shambulio hilo ulilengwa msikiti na watu kadhaa wameuawa…
No comments:
Post a Comment