Rais wa Uturuki
Erdogan ameibuka mshindi katika kura ya maoni ya
kihistoria Jumapili(16.04.2017) itakayoimarisha madarakani yake, na
matokeo hayo yameiacha nchi hiyo ikigawanyika mno na upinzani
unalalamikia udanganyifu.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Mabadiliko hayo makubwa ya katiba yaliyoidhinishwa kupitia
kura hiyo ya maoni yanaunda mfumo wa madaraka ya rais ambao
utampa rais Erdogan madaraka zaidi kuliko kiongozi yeyote tangu
muasisi wa Uturuki Mustafa Kemal Ataturk na mrithi wake Ismet Inonu.
Kambi
ya "ndio" imeshinda kwa asilimia 51.4 ya kura dhidi ya asilimia
48.6 kwa upande wa "hapana", tume ya uchaguzi imesema katika
tarakimu zilizonukuliwa na shirika la habari la Anadolu, katika
zoezi la kuhesabu kura kwa misingi ya asilimia 99.5 ya
masanduku ya kura. Watu waliojitokeza kupiga kura ni asilimia 85.
Watu wakipunga bendera wakifurahia ushindi wa Erdogan
Matokeo
ya kura hiyo pia yanaathari pana kwa Uturuki ambayo imejiunga
na jumuiya ya kujihami ya NATO mwaka 1952 na katika kipindi cha
mwisho cha nusu karne nchi hiyo imelenga katika kujiunga na
Umoja wa Ulaya.
Sherehe mitaani
Kundi
kubwa la watu waliokuwa wakipunga bendera walisherehekea ushindi
huo mitaani, Erdogan akiisifu Uturuki kwa kuchukua "uamuzi wa
kihistoria".
Mifuko ya kura kutoka katika vituo vya kupigia kura nchini Utruki
"Pamoja na umma, tumeweza kufikia mabadiliko muhimu katika historia yetu," ameongeza.
Lakini
waungaji mkono wa upinzani katika wilaya zinazompinga Erdogan za
mjini Istanbul wameonesha kutoridhishwa kwa kupiga mabakuli na
sufuria kwa vijiko na umma na kufanya kelele za kupinga. Mamia
ya watu pia waliingia mitaani katika maeneo ya Besiktas na
Kadikoy.
Mkuu wa mamlaka kuu ya uchaguzi Sadi Guven
amethibitisha kwamba kambi ya "ndio" imeibuka mshindi, lakini
upinzani umeapa kupinga matokeo hayo.
Kura hiyo ya maoni
ilifanyika chini ya amri ya hali ya hatari ambayo imeshuhudia
watu 47,000 wakikamatwa katika ukandamizaji baada ya jaribio
lililoshindwa la mapinduzi dhidi ya Erdogan Julai mwaka jana.
Waziri mkuu wa Uturuki na kiongozi wa chama tawala cha AKP Binali Yildirim
Mwishoni
mwa kampeni iliyokuwa na hamasa nyingi , kambi ya "hapana"
iliweza kuongeza idadi ya kura wakati kura zaidi zikihesabiwa ,
baada ya kuwa nyuma kwa muda mrefu katika matokeo ya awali,
lakini kambi hiyo ilishindwa kuipita kambi ya kura za "ndio".
Wakati
huo huo theluthi mbili ya Waturuki wanaoishi nchini Ujerumani
wamepiga kura zao wakimuunga mkono rais Recep Tayyip Erdogan
katika kura ya maoni inayotaka kumpa madaraka zaidi rais.
Asilimia 63.1 ya wapigakura Waturuki nchini Ujerumani wameunga
mkono hatua hiyo, limesema shirika la habari la Uturuki Anadolu
mapema leo Jumatatu.
Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker
Maoni ya viongozi mbali mbali
Taarifa
ya pamoja ya rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Calude
Juncker na waziri mwenye dhamana ya masuala ya kigeni katika
Umoja huo Federica Mogherini imesema , mabadiliko ya katiba na
hususan utekelezaji wake utatathminiwa kwa misingi ya jukumu la
Uturuki kama nchi inayotaka kujiunga na Umoja huo na mwanachama
wa baraza la Ulaya.
No comments:
Post a Comment