Viongozi wa Umoja wa ulaya wameanza mazungumzo yao
pamoja na viongozi wenzao wa bara la Afrika kuhusu uhamaji, wakipania
kuupatia ufumbuzi mzozo wa watu wanaoyatia hatarini maisha yao kwa lengo
la kuingia barani Ulaya.
Viongozi kutoka Ufaransa, Ubeigiji, Luxemburg, wote wakiwa ni
viongozi wa kiume wenye umri unaokurubia miaka 40 wanajaribu
kujitenganisha na picha ya wakoloni wa zamani wa Afrika, wakitetea
umuhimu wa kuendeleza biashara na kuwekeza katika miradi ya maendeleo na
usalama barani humo pamoja na kushughulikia vyanzo vya uhamaji.
Uhamaji
ndio mada kuu katika mkutano huu wa kilele mjini Abidjan, mji mkuu wa
kibiashara wa Côte d'Ivoire, mada iliyopata nguvu kutokana na kanda ya
video iliyotangazwa hivi karibuni na kituo cha televisheni cha CNN na
kuonyesha jinsi vijana wa kiafrika walivyokuwa wakiuzwa kama watumwa
katika masoko ya mnada nchini Libya. Akizungumza kuhusu kisa hicho cha
karaha, kansela Angela Merkel amesema:"Mada ya uhamaji kinyume na sheria
inakamata nafasi muhimu katika bara lote la Afrika wakati huu tulio nao
kwasabau kuna rirpoti zinazosema vijana wa kiafrika wamekuwa wakiuzwa
kama watumwa nchini Libya. Na hiyo ndio sababu mada hiyo inazusha jazba
kubwa katika mkutano huu. Kwa hivyo yameibuka masilahi ya pamoja ya
kukomesha uhamaji kinyume na sheria na kuwafungulia njia watu kutoka
Afrika kuweza kuja Ulaya kusoma au kujifunza kazi."
Kansela Angela Merkel akizungumza na mwenyeji wakle, rais Alassane Ouattara wa Côte d'Ivoire
Biashara ya watumwa ni uhalifu dhidi ya ubinaadam
Kansela
Merkel amesema hayo mwanzoni mwa mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja
wa ulaya na Afrika mjini Abidjan. Jana usiku rais wa Ufaransa Emmanuel
Macron aliitaja biashara ya wahamiaji wa kiafrika kuwa "uhalifu dhidi ya
ubinaadam. Macron amesema anataka nchi za Ulaya na zile za Afrika
ziwasaidie watu waliokamwa nchini Libya ili waweze kurejeshwa makwao.
Aliahidi kufafanua zaidi kuhusu juhudi hizo katika mkutano huu wa kilele
ulioanza hivi punde mjini Abidjan.
Meli ya kuwaokoa wakimbizi wa Afrika wanaoelekea Ulaya kupitia bahari ya kati
Viongozi vijana wa Ulaya wanataka kuondokana na sura ya wakoloni wa zamani
Waziri
mkuu wa ubeligiji, Charles Michel amewahimiza viongozi wenzake wa Ulaya
washirikiane kwa dhati zaidi na wenzao wa Afrika katika suala la
uhamaji na usalama, mada ya pili muhimu itakayojadiliwa katika mkutano
huu wa kilele wa siku mbili mjini Abidjan.
Tunachokitaka ni
mkakati utakaoleta manufaa kwa pande zote mbili amesema Michel mwenye
umri wa miaka 41. Ameongeza kusema anatoka katika kizazi
kinacholiangalia bara la Afrika kama mshirika, hakuna upenu katika
kizazi chetu wa kufikiria yaliyotokea zamani" amesema waziri mkuu huyo
wa Ubeligiji aliyefuatana na mwenzake wa Luxemburg Xavier Bettel,
wakionyesha sura tofauti na ile ya walio watangulia.
No comments:
Post a Comment