Watu 16 wameuawa na wengine 24 kujeruhiwa
katika matukio 56 ya kupigana risasi kiholela yaliyotokea katika kipindi
cha masaa 24 kwenye maeneo tofauti ya Marekani.
Kituo cha kutoa takwimu za
mashambulizi ya silaha nchini Marekani kimetangaza habari hiyo na
kuongeza kuwa mauaji na mashambulizi hayo yametokea katika kipindi cha
masaa 24 yaliyopoita katika majimbo ya Florida, Michigan, Texas, Ohio na
Pennsylvania.
Kwa mujibu wa kituo hicho cha Marekani,
katika kipindi cha masaa 48 yaliyopita, kumeripotia matukio 164 ya
kupigana risasi kiholela katika kona mbalimbali za Marekani ambayo
yamepelekea watu 45 kuuawa na wengine 88 kujeruhiwa.
Takwimu zinaonesha kuwa, jamii ya
Marekani ndiyo yenye silaha nyingi zaidi zinazomilikiwa na watu
majumbani kuliko jamii nyingine yoyote duniani kiasi kwamba kati ya kila
watu 100, 90 kati yao wana silaha nyepesi majumbani mwao.
Takwimu zinaonesha pia kuwa makundi ya
utengenezaji silaha yana nguvu sana nchini Marekani na ndiyo
yanayodhibiti vyama vya Democrats na Republican, hivyo serikali yoyote
inayoingia madarakani haina nguvu ya kupiga marufuku umilikaji silaha
ovyo nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment