Duru zenye uhusiano na familia ya Katibu Mkuu
wa Jumuiya ya Kitaifa ya al-Wifaq nchini Bahrain, zimeeleza kuwa
utawala wa Aal-Khalifa umemwekea vizuizi vikubwa Sheikkh Ali Salman na
shakhsia wengine mashuhuri wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa habari hiyo, Sheikh
Ali Salman na shakhsia wengine wakubwa wanaoshikiliwa katikka jela za
Bahrain wamezuiliwa kufanya mawasiliano na watu wa familia zao, kupiga
simu au hata kusoma magazeti. Katika kuendelea kutolewa hukumu za
kidhalimu za utawala wa Aal-Khalifa dhidi ya Sheikh Ali Salman
anayeendelea kutumikia kifungo cha miaka tisa jela, utawala huo
umewasilisha mahakamani mashitaka mapya dhidi ya shakhsia huyo ya kile
kinachotajwa kuwa eti ni kufanya ujasusi kwa maslahi ya Qatar.
Katika uwanja huo, mwendesha mashtaka wa
Manama amewasilisha mashtaka hayo dhidi ya Sheikh Ali Salman, Hassan
Sultwan na Ali al-Usud, ambao nao pia ni wanachama wa Jumuiya ya Kitaifa
ya al-Wifaq kwa tuhuma hizo hizo za kufanya ujasusi kwa ajili ya Qatar
kwa lengo la kile alichokisema kuwa eti ni kutaka kuiondoa madarakani
serikali ya Bahrain. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hukumu dhidi ya
shakhsia hao itatolewa tarehe 27 Novemba mwaka huu.
Sheikh Ali Salman alikamatwa mwaka 2014
na utawala wa kidikteta wa Aal-Khalifa na kuhukumiwa kifungo cha miaka
minne jela mwaka 2015 kwa tuhuma za uchochezi na kuivunjia heshima
Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo. Hata hivyo mahakama ya rufaa ya
nchi hiyo na katika njama za kutaka kumfunga miaka mingi zaidi shakhsia
huyo ilimbadilishia mashitaka na kuyafanya ya tuhuma za kutaka
kubadilisha utawala na hivyo ikamuhukumu kifungo cha miaka tisa jela.
No comments:
Post a Comment