Idadi ya waliouawa katika shambulio la Mogadishu, Somalia yafikia 358
Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la
kigaidi la siku ya Jumamosi iliyopita katika mji mkuu wa Somalia,
Mogadishu imeongezeka na kufikia 358.
Waziri wa Habari wa Somalia Abdurahman Othman ametangaza kuwa
kuwa kwa mujibu wa taarifa za karibuni kabisa kuhusu waathirika wa
shambulio la kigaidi la mjini Mogadishu, watu wasiopungua 358 wameuawa,
228 wamejeruhiwa na wengine 56 hawajulikani waliko hadi sasa.
Abdurahman Othman ameongeza kuwa majeruhi 122 wa shambulio hilo la
kigaidi wamesafirishwa kupelekwa Uturuki, Sudan na Kenya kwa ajili ya
kupatiwa matibabu.
Shambulio hilo la tarehe 14 Oktoba lililofanywa kwa kutumia lori
lililotegwa bomu lilitokea katika eneo la kibiashara la Hodan lenye
msongamano mkubwa wa watu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Majengo na magari yaliyokuweko umbali wa mita mia kadhaa yaliharibiwa
vibaya na mripuko mkubwa uliosababishwa na bomu hilo na watu wengi
waliteketea kwa moto wakiwa hai au miili yao kukatika vipande vipande.
Kabla ya shambulio la siku ya Jumamosi iliyopita, shambulio kubwa
zaidi la kigaidi kutokea nchini Somalia lilikuwa la mwezi Oktoba mwaka
2011 ambapo watu 82 waliuawa na wengine 120 walijeruhiwa.
Ijapokuwa hadi sasa hakuna mtu au kundi lolote lililotangaza kuhusika
na shambulio hilo lakini viongozi wa serikali ya Somalia hawana shaka
kuwa kundi la kigaidi na kitakfiri la Al Shabab ndilo lililofanya
shambulio hilo...
No comments:
Post a Comment