Rais Rouhani alipoonana na balozi wa Tanzania, Bw. Mbarouk Nassor Mbarouk
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema
kuwa, Tanzania ni lango muhimu la kuingilia eneo la mashariki mwa Afrika
na kwa kuzingatia kuwa Iran ina nafasi na uwezo mkubwa katika sekta
mbalimbali na jambo hilo linaufanya wajibu wa kuimarishwa uhusiano wa
nchi mbili kuwa na umuhimu wa kieneo.
Rais Rouhani amesema hayo leo
Jumamosi hapa Tehran wakati alipopokea hati za utambulisho za Balozi
mpya wa Tanzania Bw. Mbarouk Nassor Mbarouk na kusisitiza kuwa, Jamhuri
ya Kiislamu ya Iran ina hamu ya kuona kiwango cha uhusiano na
ushirikiano wake na Tanzania kinakuwa kikubwa.Mheshimiwa Rais pia amesema, kuna nyuga nyingi za kustawisha uhusiano wa Iran na Tanzania kama vile sekta ya madini na nishati na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuipatia Tanzania uzeofu wake katika masuala mbalimbali.
Kwa upande wake, Balozi Mbarouk ameashiria namna Tanzania inavyolipa umuhimu mkubwa suala la kuimarisha uhusiano wake wa Iran katika sekta tofauti na kusema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imepiga hatua nzuri katika nyuga nyingi na tofauti; za kisayansi, kiufundi na kiteknolojia hususan sekta na nishati na kwamba anaamini kuwa, Tanzania inaweza kufaidika na uzoefu wa Iran katika mambo tofauti.
No comments:
Post a Comment