Mkuu wa misaada ya kibinadamu katika Umoja wa
Mataifa amesema hali ya kibinadamu nchini Yemen ni ya kushtua huku
Saudi Arabia ikiendeleza hujuma dhidi ya nchi hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a, Mark Lowcock
ambaye Jumamosi ya leo amemaliza safari ya siku tano nchini Yemen
amesema kuwa, njia pekaa ya kumaliza vita Yemen ni kupitia mchakato wa
kisiasa.
Lowcock
amesema hali ya kibinadamu inazidi kuzorota huku ugonjwa wa
kipindupindu ukienea kwa kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa duniani.
Amesema Yemen inakabiliwa na ukosefu mkubwa zaidi wa chakula duniani na
kwamba idadi kubwa ya watu wamelazimika kuwa wakimbizi.
Vita vamizi vya Saudia na waitifaki wake dhidi ya Yemen vilianzishwa
mwezi Machi mwaka 2015 kwa kisingizio cha kutaka kumrejesha madarakani
rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abd Rabbuh Mansur Hadi.
Vita hivyo vingali vinaendelea kwa mwaka wa tatu sasa bila ya utawala
wa Aal Saud na waitifaki wake kufikia malengo haramu waliyokusudia. Watu
zaidi ya 13,000 , wengi wakiwa ni wanawake na watoto, wameuawa katika
hujuma ya Saudia nchini Yemen.
No comments:
Post a Comment