Gazeti la Kifaransa la Le Monde limeripoti
kuwa Marekani imepanua wigo wa uingiliaji wake kijeshi katika nchi za
Afrika kwa kuongeza idadi ya askari wake walioko kwenye nchi za bara
hilo.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika muendelezo wa sera za
Washington za kudhamini maslahi yake, idadi ya askari wa Marekani
wanaopelekwa katika nchi za Afrika kwa anuani ya "utoaji mafunzo,
uratibu wa majeshi ya nchi za Kiafrika na kushiriki katika mapambano
dhidi ya makundi ya kigaidi" imeongezeka mara tatu katika kipindi cha
miaka mitatu iliyopita.
Le Monde limeongeza kuwa, katika harakati inayolenga kudhamini
manufaa na maslahi yake barani Afrika, Marekani imekuwa ikivuruga
uthabiti ndani ya nchi za bara hilo ili kuongeza idadi ya vikosi vya
jeshi lake, kiasi kwamba baada ya Mashariki ya Kati, bara Afrika
limekuwa eneo la pili lenye uingiliaji mkubwa zaidi wa kijeshi wa
Marekani duniani.
Kwa mujibu wa viongozi wa Marekani, kati ya askari elfu nane wa
kikosi maalumu cha nchi hiyo ambao tangu ulipoanza mwaka huu wa
2017 wametumwa katika pembe mbalimbali za dunia, zaidi ya askari 1,300
wako barani Afrika na wengine karibu 5,000 wako katika eneo la Mashariki
ya Kati.../
No comments:
Post a Comment