Wafungwa wa jela yenye ulinzi mkali ya Tora
mjini Cairo Misri wameanza mgomo wa kula chakula wakipinga mazingira
mabaya yanatotawala jela hiyo.
Zaidi
ya wafungwa elfu moja wa jela hiyo maarufu kwa jina la Jela la Nge
wamenza mgomo wa kula wakilalamikia kunyimwa haki zao za kimsingi ikiwa
ni pamoja na kuzuiwa jamaa zao kuwatembelea, kunyimwa huduma za afya na
kadhalika.
Wakili
Usama Biyumi anayeshughulikia kesi za wafungwa kadhaa wa jela hiyo
amesema kuwa, ukatili wa idara ya jela hiyo dhidi ya wafungwa
unaongezeka siku baada ya siku licha ya matakwa ya kukomeshwa mienendo
hiyo.
Anesema kuwa maafisa wa jela hiyo wamekuwa wakizuia kuingizwa chakula kwa wafungwa na kupewa vyakula visivyokuwa salama.
Biyumi ameongeza kuwa, mgomo huo ulianzishwa siku kadhaa zilizopita
na baadhi ya wafungwa, na wafungwa wengine wa jela hiyo wamejiunga na
wenzao hao baada ya matakwa yao kukataliwa na idara ya jela hiyo.
Wafungwa
wa jela hiyo wananyimwa haki za kimsingi na manyanyaso yanashadidi
zaidi kwa wafungwa wa kisiasa ambao wanashikiliwa katika seli zenye giza
totoro na wanazuiwa kuzungumza na wenzao.
Misri
imekuwa ikikosolewa na mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za
binadamu kutoka na ukatili na manyanyaso yanayofanywa dhidi ya wafungwa
katika jela za nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment