Wapiga kura nchini Ufaransa wamerudi tena vituoni Jumapili (11.06.2017) kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge ambayo inatabiriwa utakipa chama cha mrengo wa wastani cha Rais Emmanuel Macron wingi wa viti bungeni.
Wapiga kura nchini Ufaransa wamerudi tena vituoni Jumapili (11.06.2017) kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge ambayo inatabiriwa utakipa chama cha mrengo wa wastani cha Rais Emmanuel Macron wingi wa viti bungeni.
Macron amekuwa akifurahia fungate ya kisiasa tokea alipomshinda mgombea wa sera kali za mrengo wa kulia Marine Le Pen na kuja kuwa rais kijana kabisa wa Ufaransa kuwahi kutokea hapo Mei 7 na kutangaza baraza la mawaziri lisilojikita katika mgawanyiko ulioko kati ya sera za mrengo wa kulia na kushoto pamoja na kuonekana kujiamini katika mikutano yake na Rais Donald Trump wa Marekani na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Lakini rais huyo amefanya nusu tu ya kazi.Chama chake cha Republique en Marche (Republic on the Move REM) ambacho amekiasisi miezi 14 tu iliopita kinahitaji kuwa na wingi wa viti katika Bunge la Taifa ili kuweza kupitisha mageuzi aliyoahidi wakati wa kampeni yake.
Uchunguzi wa maoni mara kadhaa umeonyesha kwamba chama cha Macron ambacho hakikuwahi kujaribiwa kinaweza kujinyakulia asilimia 30 ya kura katika duru ya kwanza na kukiweka katika njia ya kunyakuwa ushindi wa kishindo katika duru ya pili Ijumapili ijayo.
Chama cha sera za mrengo wa kati kulia cha Republicans na kile cha Socialist vinahofia kushindwa vibaya baada ya wagombea wao kushindwa kufikia ngazi ya marudio ya uchaguzi wa rais kwa mara ya kwanza katika historia ya Ufaransa baada ya kipindi cha vita.
REM yatabiriwa kupata wingi wa viti
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa akisalimiana na watu.
Baadhi ya utabiri unaashiria kwamba chama cha REM kinaweza kushinda kama viti 400 katika bunge hilo lenye viti 477 kutokana na azma ya wapiga kura kutaka kumpa rais huyo mpya mamlaka yenye nguvu.
Chama hicho tayari kinaongoza katika majimbo ya uchaguzi 19 kati ya 11 ya himaya za Ufaransa nchi za nje ambayo yamefanya duru yao ya kwanza ya uchaguzi mwishoni mwa juma lililopita.
Hapo Jumapili Macron baada ya kusalimana kwa kupeana mikono na watu waliomtakia heri na kupiga nao picha za simu ya mkononi alipiga kura yake katika mji wa kitalii wa kaskazini wa Le Touqet ambapo yeye na mke wake mwenye umri wa mika 64 Brigitte wana nyumba yao.
Usalama waimarishwa
Zoezi la kupiga kura ya bunge.
Wabunge wachache wanatazamiwa kuchaguliwa katika duru ya kwanza.Iwapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50,wagomea wawili wa juu wanaongoza wataingia duru ya pili sawa na mgombea aliyejikusanyia angalau asilimia 12.5 ya wapiga kura waliojiandikisha.
Vituo vya kupiga kura katika miji mkubwa vitakuwa wazi hadii saa mbili usiku ambao matokeo ya awali yataanza kutolewa muda mfupi baada ya hapo.
Kufikia mchana asilmia 19.24 miongoni mwa wapiga kura milioni 47 wanaostahili kupiga kura ilikuwa imejitokeza ikiwa ni chini kwa asilimia 21.06 katika wakati kama huo wakati wa uchaguzi wa bunge mwaka 2012.
Zaidi ya polisi 50,000 walikuwa katika doria katika nchi ambayo bado iko katika wasi wasi baada ya wimbi la mashambulizi ya wapiganaji wa jihadi kuuwa zaidi ya watu 230 tokea mwaka 2015.
Katika tuko la hivi karibuni kabisa Mualgeria aliyejipandikiza itikadi kali mwenye umri wa miaka 40 alipigwa risasi na kujeruhiwa baada ya kumshambula polisi na nyundo nje ya kanisa la Notre Dame mjini Paris.
No comments:
Post a Comment