Wapinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo wanasema mazungumzo ya namna Rais Joseph Kabila (pichani) atakavyoondoka
madarakani yanalegalega na yamkini yakasambaratika.
Kwa
mujibu wa Félix Tshisekedi mmoja kati ya vinara wa upinzani, pande
husika katika mazungumzo hayo zinakaribia kusambaratika kuliko kupata
suluhisho.
Leo
mazungumzo baina ya serikali na vyama vya upinzani chini ya upatanishi
wa Kanisa Katoliki yamefanyika mjini Kinshasa. Jana Alhamisi makasisi
wapatanishi walikutana na Rais Kabila pamoja na kiongozi mkongwe wa
upinzani Etienne Tshisekedi ili kujaribu kufikia mwafaka.
Kwa
mujibu wa mapatano yaliyopendekezwa, Kabila hatabadilisha katiba ili
ashiriki katika uchaguzi mkuu mwakani. Aidha utawala wake wa mihula
miwili ambao ulimalizika Disemba 19 utaongezwa hadi mwaka 2018.
Etienne Tshisekedi |
Hata hivyo kizingiti kikuu kimeripotiwa kuwa ni iwapo waziri mkuu atoke mrengo mkuu wa upinzani. Aidha kumekuwepo mvutano kuhusu Tume ya Uchaguzi ambayo wapinzani wanasema inaegemea upande wa serikali.
Watu
40 walipoteza maisha wiki jana mjini Kinshasa katika maandamano ya
kutaka Kabila aondoke madarakani baada ya kuitawala nchi hiyo tokea
mwaka 2001 wakati baba yake, Laurent Desire Kabila, alipouawa.
No comments:
Post a Comment