SHIRIKA
la Ndege la Etihad kupitia Kitengo chake cha Uhandisi (Etihad Airways
Engineering) kwa kushirikiana na Lental Textiles AG wamezindua maabara
ya kipekee ya kwanza Mashariki ya Kati kwa ajili ya wateja wa kanda hiyo
walio sekta ya anga na waendeshaji mashirika ya uzalishaji na
ubunifu.Maabara hiyo ambayo ipo ndani ya kituo cha uhandisi cha Shirika
la Ndege la Etihad karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abu
Dhabi itakuwa inatoa huduma mbalimbali ikiwemo vipimo vya kuwaka kwa
moto, joto, moshi n.k.
Aidha,
maabara hiyo itaenda sambamba na hadhi ya ubora wa Kimataifa ISO 17025
na vipimo vyote vitafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Anga za imataifa
FAR/CS25.853.
Kwa
mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la
Ndege la Etihad Jeff Wilkinson alisema, “Tunatoa huduma zilizotukuka
kwenye matengenezo ya ndege na ufumbuzi wa kiuhandisi katika soko la
anga duniani na kwa ajili ya aina zote za ndege za kibiashara.
“Kupitia
ushirikiano wetu huu na Lantal, itakuwa rahisi sasa na haraka kwa kwa
wateja wa sekta ya anga katika Ukanda kupata huduma bora za vipimo
katika kituo chetu cha Abu Dhabi,” alisema.
Naye
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Lantal, Dkt. Urs Rickenbacher alisema, “Maabara
yetu ya Lantal kwa ajili ya vipimo nchini Uswisi inajulikana vema kwa
huduma zake bora na haraka. Kwa sasa tunalo soko kubwa barani Ulaya na
sasa maabara yetu hapa Abu Dhabi tukishirikiana na Kitengo cha Uhandisi
cha Shirika la Ndege la Etihad (Etihad Aiways Engineering) litatuwezesha
kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wateja wetu wa Mashariki ya Kati,”.
No comments:
Post a Comment