Ripoti kutoka Misri zinaeleza kuwa licha ya
malalamiko ya wananchi na upinzani wa mahakama, serikali ya nchi hiyo
imepitisha mpango wa kuipatia Saudi Arabia visiwa viwili vya Tiran na
Sanafir.
Duru za habari za Misri zimetangaza kuwa serikali imeidhinisha mpango
huo na tayari imeshaupeleka bungeni.
Kwa
mujibu wa duru hizo, Mahakama Kuu ya Misri imepinga mpango huo na
inatazamiwa kutoa hukumu yake rasmi juu ya suala hilo katika kipindi cha
wiki mbili zijazo.
Baadhi
ya shakhsia na wataalamu wa sharia nchini Misri wanaitakidi kuwa uamuzi
wa kupitishwa mpango wa kuipatia Saudia visiwa viwili ambavyo Wamisri
waliowengi wanaamini ni milki ya nchi yao una uhusiano na kadhia ya
kamati za sharia za bunge la Misri.
Ahmad
Suleiman, waziri wa zamani wa sharia ameashiria suala hilo na kueleza
kwamba lengo la mpango huo ni kukabiliana na mahakimu wanaotoa hukumu
kinyume na matakwa ya viongozi wa serikali na badala yake kuzingatia
maslahi ya taifa tu. Ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuwaondoa
mahakimu wanaotoa hukumu zisizoendana na mitazamo ya serikali.
Mapema mwaka huu, serikali ya Misri ilitiliana saini mkataba wa
mipaka ya bahari na Saudia na kutangaza kufuatia hatua hiyo kwamba
visiwa vya Tiran na Sanafir viko kwenye maji ya ardhi ya Saudia.
Imeelezwa
kuwa serikali ya Cairo itapatiwa dola bilioni 20 na Saudi Arabia kwa
kuupatia utawala wa kifalme wa Aal Saud visiwa hivyo.
Uamuzi
huo umelaaniwa na kulalamikiwa vikali na wananchi, duru za kisiasa,
vyombo vya habari na asasi za kiraia nchini Misri ambao wamemtuhumu Rais
Abdel Fattah el Sisi kuwa amefanya uhaini na kuziuza ardhi za nchi
hiyo.
Hata
hivyo katika jibu alilotoa kuhusiana na tuhuma hizo El Sisi amesema
hajaipatia Saudia hata chembe ya ardhi ya Misri bali ameirejeshea nchi
hiyo haki yake…/
No comments:
Post a Comment