Waandishi wa habari wakiwa kwenye moja ya harakati za kuripoti matukio kwenye eneo la Israel na Palestina
Waandishi wa habari 65 na wafanyakazi wa vyombo vya
habari wameuawa katika mwaka 2017, hii ni kwa mujibu wa ripoti
iliyochapishwa na shirika la wanahabari wasio na mipaka RSF.
Miongoni mwao 50 walikuwa ni maripota, hii ikiwa ni idadi ndogo zaidi katika kipindi cha miaka 14.
Hata hivyo ripoti
inasema kuwa huenda kupungua kwa idadi ya vifo vya wanahabari imetokana
na waandishi na ripota wengi kuacha kuripoti habari kwenye maeneo yenye
vita.
Nchi ya Syria ambao kwa
zaidi ya miaka 6 imeshuhudia vita vya wenywe kwa wenyewe, imesalia kuwa
nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari kufanya kazi, imeonesha ripiti
ya RSF ambayo imesema waandishi wa habari 12 waliuawa nchini humo,
ikifuatiwa na Mexico ambako 11 waliuawa.
Miongoni mwa waliouawa
nchini Mexico ni mwanahabari maarufu wa habari za biashara haramu ya
dawa za kulevya nchini humo Javier Valdez ambaye mauaji yake
yalitamausha wengi.
Waandamanaji nchini Kenya wakiwarushia mawe polisi na waandishi wa
habari, waliokuwa wakiripoti maandamano ya kupinga vitendo vya rushwa,
Nairobi, 3 Novemba, 2016.REUTERS/Thomas Mukoya
Mwandishi mwingine wa habari wa shirika la AFP aliuawa kwa kupigwa risasi nchini Mexico katika mji wa Kaskazini wa Sinaloa.
Nchi ya Ufilipino
imekuwa ni taifa jingine hatari kwenye ukanda wa Asia kwa waandishi wa
habari kufanya kazi ambapo ripiti inaonesha waandishi wa habari watano
waliuawa kwa kupigwa risasi mwaka uliopita.
Ongezeko hili lilitokana
na matamshi ya rais Rodrigo Duterte ambaye alisema “haimaanishi ukiwa
muandishi wa habari basi ndio usiuawe ikiwa unajihusisha na biashara
haramu”.
Hata hivyo hakukuwa na mwanahabari aliyeuawa mwaka uliotangulia nchini Ufilipino.
Waandishi wa habari nchini Misri wakiwa wamebeba kamera zao nje ya ofisi ya chama cha waandishi wa habari Reuters
Kiujumla ripoti ya RSF inasema kuwa idadi ya vifo vya wanataaluma wa habari imepungua kidunia katika kipindi cha miaka 14.
Katika vifo vya
wanahabari 65, ripoti inaonesha kuwa wanahabari 39 waliuawa huku wengine
wakipoteza maisha wakiwa kwenye majukumu yao ya kazi kama vile
mashambulizi ya anga au yale ya kujitoa muhanga.
RSF inasema kuwa huenda pia vifo vimepungua kutokana na waandishi wengi wa habari kutopokea mafunzo ya kujilinda wakati wa vita.
Nchi ya Uturuki inatajwa
kwenye ripoti hii kwa kuwa na magereza mengi ambayo waandishi wa habari
wanashikiliwa, ambapo kwa sasa zaidi ya wanahabari 42 wanazuiliwa.
Nchi nyingine
zinazofunga waandishi wa habari kwenye jela zake ni pamoja na Syria
ambako kuna wanahabari 24, Iran wapo 23 na Vietnam ambako wako 19.
No comments:
Post a Comment