Tanzania na Rwanda zimeunganisha nguvu
kupitia majeshi yao ya polisi chini ya wakuu wake IGP Simon Sirro wa
Tanzania na Emmanuel Gasana wa Rwanda ili kupambana na uhalifu, ujangili
na kuangalia namna ya kutatua matatizo ambayo yanazikumba nchi hizo.
Akizungumza na Waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam Emmanuel Gasana, Mkuu wa Jeshi la Polisi la
Rwanda amesema kuwa, lengo ni pande mbili kushirikiana kutokana na
changamoto ambazo zinatokea katika nchi mbili hizo likiwemo suala la
kuongeza nguvu, teknolojia, vifaa na kuongeza uzoefu wa matumizi ya
vifaa.
Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini Tanzania IGP Simon Sirro amesema kuwa, ushirikiano huo
unafanyika kwa kuangalia nini ambacho kinatakiwa kufanywa na maarifa
ambayo yatatumiwa ili Jeshi la Polisi liweze kufanya kazi yake kwa
usahihi na kupunguza uhalifu na endepo mtu akijiingiza kwenye uhalifu
anaweza kupoteza familia yake na kuishia pabaya.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Tanzania IGP Simon Sirro amesema kuwa, “Wenzetu Rwanda wako mbele katika
matumizi ya teknolojia, hivyo kuna baadhi ya mambo ambayo watatuelekeza
na tutapata uzoefu katika kupambana na wahalifu wa mitandaoni ambao
wamekuwa wakiwasumbua raia katika nchi yetu.
Aidha IGP Simon Sirro ameongeza kuwa,
sisi pia tuna uzoefu wa mambo mengi ambayo wenzetu Rwanda watajifunza
kutoka kwetu na hivyo tunaweza kusema kuwa, kila mmoja katika
ushirikiano huo anaweza kumpatia mwenzake uzoefu alionao hasa katika
suala zima la kupambana na uhalifu
No comments:
Post a Comment