Jeshi na kamati za kujitolea za wananchi wa
Yemen zimeshambulia kwa kombora la belestiki komandi wa kijeshi ya
wanajeshi vamizi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika mkoa wa
Ma'rib nchini Yemen.
Mwaka 2015, Saudi Arabia kwa
kushirikiana na baadhi ya nchi za Kiarabu hasa Imarati na kwa baraka
kamili za Marekani, Israel na baadhi ya madola ya Magharibi ilianzisha
mashambulizi makubwa ya kila upande katika nchi maskini ya Yemen. Hadi
hivi sasa makumi ya maelfu ya wananchi wa nchi hiyo ya Waislamu
wameshauawa na kujeruhiwa na mamilioni ya wengine wamekuwa wakimbizi.
Wananchi wa Yemen kupitia jeshi lao na
kamati za kujitolea vya wananchi wamelazimika kujihami na kusimama
kidete kupambana na wavamizi wa nchi yao, hivyo wamekuwa mara kwa mara
wakijibu mashambulizi wanayofanyiwa.
Maarib
Televisheni ya al Masira ya Yemen
imetangaza kuwa, katika opereseheni ya jana Ijumaa, vikosi vya Yemen
vilishambulia kwa kombora la balestiki komandi ya kijeshi ya wanajeshi
vamizi wa Imarati katika mkoa wa Ma'rib, katikati mwa Yemen.
Vile vile jeshi la Yemen na kamati za
kujitolea za wananchi zimefanikiwa kuangamiza mamluki 18 wa Saudia na
kujeruhi makumi ya wengine katika eneo la al Sarwah, mkoani Ma'rib.
Itakumbukwa kuwa juhudi mbalimbali
zinaendelea kwa shabaha ya kukomesha uvamizi na mashambulizi ya kikatili
ya kundi vamizi la nchi zinazoongozwa Saudia huko Yemen. Kwa upande
wake, harakati ya Answarullah ya Yemen imependekeza kuundwa kamati
maalumu ya mapatano na kupewa nafasi wananchi kutumia haki yao ya
kidemokrasia ya kuchagua rais na wabunge kwa namna ambayo wananchi na
vyama vyote vya kisiasa vya Yemen vitashiriki kwa uhuru kamili kwenye
chaguzi hizo.
No comments:
Post a Comment