Waislamu 400 wafariki dunia Myanmar katika kipindi cha wiki moja
Waislamu takribani 400 wamefariki dunia nchini Myanmar katika kipindi cha wiki moja tokea jeshi la nchi hiyo lianzishe kampeni mpya ya kuwakandamiza Waisalmu wa jamii ya Rohingya.
Takwimu ramsi zinaonyesha kuwa watu 400 wamepoteza maisha katika jimbo la Rakhine tokea Ijumaa iliyopita. Kati ya walipooteza maisha ni wale waliouliwa na jeshi la nchi hiyo katika oparesheni dhidi ya Waislamu huku wengine, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, wakipoteza maisha wakati wakivuka mto kukimbia mapigano katika jimbo la Rakhine.
Jeshi la Myanmar Ijumaa iliyopita lilianzisha oparesheni kali dhidi ya Waislamu kwa madai kuwa watu wanaodaiwa kuwa ni Waislamu walihujumu vituo vya polisi jimboni Rakhine.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, Waislamu wa kabila la Rohingya ni jamii ya wachache inayodhulumiwa na kunyongeshwa zaidi duniani.
Katika miaka ya karibuni, Waislamu wengi wa kabila la Rohingya nchini Myamnar wameuawa au kulazimika kuhama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi za Bangladesh, Thailand, Malaysia na Indonesia kutokana na mashambulio ya Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mpaka wanaoungwa mkono na serikali ya nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment